Leo tar, 9.12.2013 Raisi J.M.Kikwete amewaongoza maelfu ya Watanzania pamoja na Wageni mbali mbali kutoka nchi za nje katika kuadhimisha Miaka 52 ya Uhuru Tanzania. Maadhimisho hayo yamefanyikia katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salam
MATUKIO KATIKA PICHA
Raisi wa Jamhuri ya muungano akiwa na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania wakiwasalimia Watanzania mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Uhuru Dar es salam
Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Tanzania wakipokea salamu ya Raisi na kupigiwa Mizinga 21 kutoka kwa Gwaride la Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania leo katika Uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili.
Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wakikagua Gwaride la Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi na Usalama leo katika uwanja wa Uhuru wakati wa Maadhimisho ya Miaka 52 ya Uhuru
Sehemu ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakiwa wamesmama kwa Ukakamavu
Baadhi ya Maofisa wa Jeshi wakipiga Saluti wakati Wimbo wa Taifa ukiimbwa
Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania . akizungumza jambo na mkuu wa majeshi
Gwaride likipita Mbele ya Raisi na Amiri jeshi mkuu kwa mwendo wa haraka
Mke wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akiwasili Jukwaa Kuu la Uwanja wa uhuru katika Maadhimisho ya Miaka 52 ya Uhuru Tanzania.
Maelfu ya Watanzania na Wageni Waliohudhuria maadhimisho hayo
Vijana wakiwasilisha Ujumbe kupitia Sanamu ya Mnyama aina ya Samba
Vijana wakionyesha Ukakamavu Mbele ya Halaiki ya Watanzania na Wageni waliohudhuria Maadhimisho
Raisi wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein {kushoto} Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh,Jakaya Mrisho Kikwete {katikati}na Mkuu wa Majeshi Generali Mwamunyange wakisoma jarida letu lililochapishwa na idara ya habari
Mheshimiwa Mbowe ni mmoja wa Watanzania waliohudhuria Maadhimisho hayo akisoma Jarida la nchi yetu
No comments:
Post a Comment