Pamoja na kuchelewa kufika katika viwanja vya CDT Kahama mjini lakini Dr Willbroad Slaa alifanikiwa kuwahutubia mamia ya wakazi wa kahama siku ya juma tano tar. 04.12.2013. Dr Slaa aliwasili Kahama Mjini mnamo saa kumi na mbili jioni Baada ya taarifa zisizo rasmi kusema msafara wake ulipata break down maeneo ya Tinde akiwa kalibu Kabisa kuingia {W}Kahama. japo muda ulikua nje ya kibali aliwataka radhi wakazi wa Kahama akiahidi kupanga ratiba ya kurudi tena kwa ajili ya kuongea na wakazi hao ambao hawakukata tamaa ya kumsubili japo walitangaziwa kua angekua katika viwanja hivyo toka saa nane mchana. aidha Dr Slaa alitumia muda mchache akiwaelezea wakazi wa kahama umuhimu wa kuheshimu katiba ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo {CHADEMA} na akisema katika chama hakuna aliye mkubwa kuliko katiba, pia aliwaahidi wanachama wa chama hicho cha Chadema kua maneno na propaganda zinazoendelea kuongelewa mitaani juu ya maamuzi yaliyotolewa na kamati kuu juu ya sakata la Mh.Zitto Kabwe na wenzake ni moja ya harakati za kuziima kabisa oparesheni ya kukisafisha chama kuelekea Ikulu Mwaka 2015.mengi utayapata katika video yake iliyopo chini ya hizi picha
Boda Boda wakishangilia Baada ya DR SLAA kuwasili viwanja vya CDT KAHAMA MJINI
wengine wakishangilia huku wakiwa mabango yaliyokua na ujumbe tofauti tofauti
Idsam Mapande {aliyevalia tisheti nyekundu}akiwa mmoja wa waliohudhuria mkutano huo
Shangwe zikiendelea
Dr Slaa akiwahutubia mamia ya wakazi waliofika eneo hilo
No comments:
Post a Comment