Huu ni mfululizo wa matukio ya sanaa ya mnato ambayo hukusanya watu wasiopungua 200 ndani ya dakika 20 kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kijamii hasa KIAFYA na KIELIMU majadiliano haya ambayo huambatana sana na uhamasishaji kwa kupitia michezo ya kuigiza hulenga kutafuta ufumbuzi wa tatizo linalokua limetokea katika jamii mfano; Gonjwa Hatari sana la UKIMWI limekua gumzo kubwa katika jamii hasa kwa kuondoa uhai wa watu wengi sana katika familia kitu ambacho kimepelekea gonjwa hili kuzungumzwa kwa hisia tofauti katika jamii,YOUTH CLUSTER ni klasta ya vijana kutoka katika mradi wa ROADS II KAHAMA unaodhaminiwa na FHI360, klasta hii ya vijana hulenga kuwapa elimu vijana wenzao walioko katika mazingira hatarishi mitaani hasa ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kupitia njia ya maigizo.
Zifuatazo ni picha za baadhi ya matukio ya SANAA MNATO ambayo hufanywa na kikundi hiki cha YOUTH CLUSTER kupitia mradi wa ROADS II ulioko {W}KAHAMA, SHINYANGA unaodhaminiwa na shirika la FHI360 karibu sana mdau
HUU NI UMATI WA WATU WALIOHUDHURIA TUKIO LA SANAA MNATO ENEO LA MUNGHULA KATA YA NYIHOGO
PICHA NYINGINE ZA MATUKIO MBALI MBALI YA SANAA MNATO KATIKA TUKIO LA MUNGHULA KATA YA NYIHOGO
watu waliofika wakieendelea kuchangia maoni yao kulia ni mwezeshaji Teach Maker
mkazi wa maeneo hayo ya mhungula akiendelea kutoa maoni yake juu ya igizo lililo chezwa
Dada aliyejitambulisha kama Recho akiendelea nae kutoa maoni yake pembeni ni mwezeshaji Teach Maker
Mdau mwingine huyo akitoa maoni yake mara baada ya mchezo wa igizo kugandishwa
Watu wakiendelea kuskiliza maoni yanayotolewa na wakazi hapo mhungula kata ya nyihogo
Anold sesemka akitoa maoni yake kupitia mchezo wa igizo lililochezwa siku hiyo Mhungula Kata ya Nyihogo
No comments:
Post a Comment